Jumapili, 25 Februari 2018

Rafid Ahmed Alwan al-Janabi, ambaye vyombo vya usalama vya Marekani na Ujerumani vilimpa jina la kificho la Curveball ndiye mtu ambaye alitumika kwa kiasi kikubwa kuithibitishia Marekani na kuharalisha propaganda za Marekani kuwa Sadam Hussein anamiliki silaha za Nyuklia. Ukitafuta neno Curveball ktk 'search engine' yoyote utaweza kujifunza mengi kuhusu uongo uliosababisha uvamizi na vifo vya wairaq zaidi ya 100,000 mpaka sasa  na bado hali ni tete.

Marekani ilitaka mtu ambaye anaweza kuthibitisha madai yao ili wapate sababu za wazi za kuishambulia Iraq, kwahiyo alipojitokeza Rafid ikawa Mungu amejibu maombi ya Marekani. Baadhi ya taarifa zinasema Rafid alitumiwa na vyama vya upinzani na makundi ya watu ambao walikuwa wakitaka Sadam Hussein aangushwe kwa gharama yoyote ile ktk kushirikiana na Marekani na Uingereza ili kuwezesha uvamizi utakaoweza kumuondoa Sadam madarakani.

Taarifa zinasema kuwa Rafid almaarufu kama Curveball ndiye 'Spy' aliyefanikiwa kuvidanganya vyombo vya ulinzi na usalama mbalimbali duniani kwa mafanikio makubwa. Lakini, wengine wanasema japo mataifa ya Marekani na Uingereza walitilia mashaka taarifa za Rafid, hawakutaka kupoteza muda maana walikuwa wamepata mwanya salama na safi kutekeleza malengo yao ya uvamizi.

Mwaka 1999 ndipo Rafid alipowasili ktk kambi ya wakimbizi ya Ujerumani na kuomba hifadhi, hapo ndipo alipoanza kuwalisha uongo uliofanana na kweli. Rafid alipohojiwa alisema kjwa "“I had the chance to fabricate something to topple the regime. I and my sons are proud of that, and we are proud that we were the reason to give Iraq the margin of democracy.”--Rafid Ahmed Alwan al-Janabi aka CURVEBALL

Kwa tafsiri isiyo rasmi" nilipata nafasi adhimu ya kutengeneza uongo unaoweza kuuangusha utawala wa kipindi hicho (Sadam Hussein), mimi na mwanangu tunajivunia hilo, na tunajivuna kwa kuwa sababu/sehemu iliyoipa Iraq utawala wa kidemokrasi "

Kwa kauli hii ya Curveball na kauli zake. nyingine nyingi unaweza kuona kuwa huenda Sadam Hussein alichukiwa na baadhi ya watu kiasi kwamba sababu yoyote hata ikiwa haramu inayoweza kumuangusha Sadam ilionekana baraka na nzuri bila kujali madhara yake.

Wakati makundi  yanayompinga Sadam pamoja na vyama vya upinzani vikimtumia Rafid ili atoe taarifa za uongo kuhusu Iraq, Marekani pia ilikuwa ikisubilia kwa hamu taarifa hiyo ya uongo ya Rafid ili waitumie kuharalisha mpango wao wa kuivamia Iraq kwa maslahi yao binafsi.

Mashirika ya kimataifa, vyama vya siasa,. makundi ya kijamii na wanaharakati wa dini waliisaidia Marekani na Uingereza kuuaminisha umma kuwa Sadam Hussein alikuwa akizalisha silaha za maangamizi/Nyukilia (Nuclear Weapons).

Propaganda zisipopingwa kwa nguvu zote, kuna ambao huziamini na kuziabudu propaganda hizo. Idadi ya watu walioziamini propaganda zao iliendelea kukua kila siku, mpaka Marekani na Uingereza walipofanikiwa kuivamia Iraq na kuhakikisha kuwa Sadam Hussein ananyongwa.

Lengo kuu la kuivamia Iraq ilikuwa kuhakikisha kuwa wanamzuia Sadam Hussein ktk kuzalisha silaha za maangamizi ambazo kwa mujibu wa Marekani walisema zipo silaha za maangamizi zilizotengenezwa zinazotishia dunia hususani mashariki ya kati. IKIWA suala la Silaha za Nyuklia ndiyo sababu kuu, ulimwengu haukutegemea pasiwepo tena na silaha za nyuklia huku wahusika wakianza kubainika kuwa walijipikia hiyo sababu ilimradi Sadam aondolewe. Hii inatoa tafsiri ya kuwa, lengo kuu ni Sadam kuondoka bila kujali kama sababu inayosemwa ina mashiko au haina, lakini kwanza atoke  hilo tunalijua leo.

Walitumia kila mbinu ktk kuuthibitishia umma wa Iraq na ulimwengu kuwa Iraq ina silaha za Nyuklia hivyo ni tishio kubwa. Lakini baada ya uvamizi kitu cha kwanza Marekani na wenzake kukidhibiti ilikuwa wizara ya mafuta, visima vya mafuta na miundombinu ya mafuta, na mpaka leo hii Marekani ina ushawishi mkubwa sana ktk nyanja hizo nchini Iraq.

Aliyekuwa Waziri wa ulinzi wa wakati huo, Collins Powell aliliambia bunge la seneti kuwa Iraq ilikuwa na silaha za Kinyuklia ambazo ni hatari, Powell alisema kuwa Rafid ambaye alikuwa ni Chemical Engineer ktk kile. kilichoitwa kuwa ni mpango wa Sadam wa kutengeneza silaha za nyuklia alikuwa na ushahidi wote na hata ushahidi kwamba watu zaidi 13 walikufa ktk moja ya vituo vya kinyuklia huko Iraq wakiwa ktk utekelezaji wa mpango huo wa kuzalisha silaha za nyuklia. Marekani dhidi ya Iraq.

Rafid aliyetumika kufanya propaganda za kuuaminisha umma kuwa kuna silaha za nyuklia Iraq baadae aikuja kukiri kuwa hakukuwa na kitu kama hicho  na kwamba eti. alidanganya ili tu Sadam angolewe madarakani. Hata hivyo waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani, Donald Rumsfeld alikwishatanabahisha kuwa Iraq haikuwa na silaha za kinyuklia.

Neno moja la. uongo la Rafid Janabi. liliipa sababu Marekani kugeuza Iraq kjwa uwanja wa vita, inakadiriwa kuwa watu zaidi ya 100,000 wamepoteza maisha tangu Marekani ilipoivamia Iraq. Makovu ya uvamizi huo yamesababisha makundi ya kiasi kuongezeka na yale yaliyokuwepk yalipata mwnya wa kupevuka na 'kunawili' mpaka leo hii ikazaliwa Isis na mengineyo, hakuna uthibiti wa serikali kwa asilimia 100 ya taifa la Iraq, kila kundi la waasi linathibiti sehemu yake huku serikali nayo ikipambana kujiimarisha bila mafanikio. Je nani ananufaika na hilo hali??

Rafid alipohojiwa na gazeti la The Times alikiri wazi kuwa yeye alidanganya ilimradi ipatikane sababu itakayowezesha Sadam kuondoka au kuondolewa madarakani kwa namna yoyote ile. Rafid hakujali kuwa wanaotaka kumuonfoa Sadam madarakani wanafanya hivyo kwa sababu ya ajenda zao binafsi, yeye hakujali ajenda za Marekani waka Uingereza, yeye. na wenzake wa upinzani walitaka Sadam atoke na alitoka.

Je silaha za maangamizi za kinyuklia ambazo walisema zinazalishwa Iraq ziliwahi kupatikana?  Baada ya uvamizi ndipo ripoti mbalimbali zinathibitisha kuwa hakukuwa na silaha za maangamizi Iraq bali ilikuwa propaganda tu.

Lakini walifanikiwa kuwatumia wairaq, mashirika, vyama vya upinzani, taasisi mbalimbali za dini kuhakikisha kuwa adui namba wa Iraq anakuwa Sadam Hussein kabla hawajavamia. Wairaq waliisaidia Marekani na Uingereza kuivamia Iraq leo wanajuta, maisha ya Iraq baada ya kuuliwa kwa Sadam Hussein ni hatari tupu zaidi ya kipindi cha Sadam Hussein.

#SomoLaKujifunza

Huenda Sadam hakutakiwa kuendelea kuwa Rais wa Iraq kwa mujibu wa wapinzani wake wa ndani na nje   huenda Sadam alikuwa dicteta asiyefaa na kwamba ilikuwa ni sawa kabisa kumuondoa madarakani lakini sababu iliyotolewa ktk uso wa dunia kuwa Iraq ina silaha za kinyuklia na sababu hiyo ndiyo ikatumika kuivamia Iraq HAIKUWA YA KWELI.

Walijua wakitumia sababu ya kweli kwamba hawamtaki Sadam Hussein kwasababu anaziba maslahi ya Marekani au Uingereza ktk mafuta nk wananchi hawawezi hata siku moja kuunga mkono hata kama Sadam Hussein alikuwa dicteta. Propaganda kuhusu silaha za Nyuklia zilifanywa kwa ustadi wa hali ya juu sana, wananchi waliambiwa kuwa Sadam akifanikiwa kutengeneza silaha za nyuklia atazitumia dhidi ya wapinzani wake wa ndani ya nchi, kauli za aina hiyo ziliwaunganisha wapinzani dhidi ya serikali na Sadam kwa kuamini kuwa Sadam ni kifo chao cha kesho. Hakuna aliyetaka kuhoji kuwa Marekani au Uingereza leo wanatuonea huruma bure? Haya mapenzi ya Marekani yameanza lini na taifa hili la kiarabu??!

Kwanini waliamua kutumia sababu ya uongo ili tu wafanikiwe kupata kibali ktk macho ya kimataifa cha kuivamia Iraq? Kwanini hawakutafuta sababu yenye ukweli ili hata baada ya miaka 100 historia isije kutambua kuwa kuna mahala watu mataifa au makundi flani yaliungana kufanya tukia kwa kutumia sababu za kupika? Hata wakitumia uongo,. ilimradi ktk kipindi cha wakati huo utaonekana kuwa ni ukweli, wakimaliza lengo lao hakuna kitakachobadilisha yatakayotokea ktk vuta au hayo malengo yao hata kama ni miaka mingapi ijayo. Hiroshima na Nagasaki yalipigwa mabomu ya atomic kwasababu zao lakini walijificha ktk vita ilihali yalikuwa majaribio mpaka leo ni vilio.

BONYEZA Magoiga SN|¦| Think Beyond Obvious

Jumamosi, 24 Februari 2018

INTELIJENSIA 10 MASHUHURI DUNIANI

Na Simon Noel

10.ASIS   AUSTRALIA
Makao makuu Canberra Australia
Nchi ya Australia ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye utulivu Wa hali ya juu.
Idara yao ya ijasusi ya ASIS imeweza kuwahakikishia wananchi wa Australia utulivu wa hali ya juu na pia Idara yao ya ujasusi ya ASIS imeweza pia kuwa Idara mashuhuri iliyoweza kudhibiti wahamiaji haramu kuingia nchini humo

9. DGSE  UFARANSA
Makao makuu Paris Ufaransa
Nchi ya Ufaransa ni miongoni mwa nchi zinazokumbwa na mashambulizi ya magaidi Mara kwa mara. Shirika lao la ujasusi la DGSE limekuwa mstari Wa mbele kuwalinda raia wake ingawa kwa siku za karibuni limeonekana kupungua uwezo wake. Shirika hili la ujasusi pia limekuwa imara kuhakikisha Ufaransa inakuwa na Amani na utulivu

8. BND UJERUMANI
Makao makuu Pullach na Berlin
Nchi ya Ujerumani ni miongoni mwa nchi zilizoendelea na hutumia bajeti kubwa sana katika maswala ya usalama hivyo basi shirika lao la ujasusi limeweza kufanya kazi kwa ufanisi na kuwahakikishia raia wao usalama na uutulivu. Kwa miaka ya karibuni shirika la ujasusi la Ujerumani limeweza kudhibiti mashambulizi ya kigaidi kutokea nchini

7 RAW INDIA
Makao makuu Delhi India.
Vita vya Mara kwa Mara na Pakistan na kuongezeka kwa uhalifu nchini humo kuliisukuma serikali ya India kuanzisha shirika la kijasusi la RAW mwaka 1968 mahsusi kabisa kulinda usalama Wa taifa lao. Kufikia wakati huu RAW ni moja ya mashirika hodari kabisa ya kijasusi duniani likiwa na majasusi sehemu mbali mbali duniani wakikusanya taarifa mbalimbali kwa usalama Wa nchi yao ya India.

6. MSS CHINA
Makao makuu Beijing
Nchi ya China ni miongoni mwa nchi zenye nguvu kubwa za kijeshi na hutumia bajeti kubwa Sana katika maswala ya usalama. Shirika la ujasusi la china limefanikiwa kuwa miongoni mwa mashirika ya kijasusi yenye weledi wa hali ya juu huku wakitumia vifaa vya kisasa na uwezo wake umeonekana kuimarika siku hadi siku

5. GRU URUSI
Makao makuu Moscow
Shirika hili liliundwa baada ya kuvunjika kwa shirika la ujasusi la KGB ambalo lilikuwa shirika la ujasusi la nchi muungano Wa soviet. Wakati Fulani KGB iliwahi kuwa Idara ya ujasusi yenye nguvu duniani ila kwa sasa GRU inashika nafasi ya tano ikizidiwa na nchi nyingine kwa weledi na ujuzi katika maswala ya ujasusi na upelelezi. GRU imesaidia sana kudhibiti uhalifu ndani ya nchi ya Urusi

4. M16 UINGEREZA
Makao makuu London
M16 Ni moja kati ya idara za kijasusi zenye miaka mingi sana. Nchi nyingi sana duniani hujifunza utawala na mifumo ya ulinzi na ujasusi kutoka nchi ya uingereza. Shirika la M16 limeweza kutoa mafunzo kwa nchi nyingi sana duniani na limeweza kufanya operesheni mbali mbali zenye mafanikio sehemu mbali mbali duniani na limeweza pia kudhibiti hali ya usalama nchini Uingereza na pia hutoa msaada Wa ulinzi katika nchi mbali mbali duniani

3. Mosad ISRAEL
Makao makuu Tel Aviv
Tangu lilipoanzishwa mpaka sasa shirika la mosad limeweka rekodi ya kufanya miujiza ya kushangaza katika operesheni zake. Wakati Wa kuokoa mateka Wa kiyahudi waliokuwa entebe mosad walifanya operesheni ya kushangaza dunia. Mmoja Wa ofisa wake alivaa kama idi Amin hali iliyowazubaisha watekaji na kupelekea operesheni hiyo kufanikiwa. Mosad pia imekuwa ikilinda kwa uhakika maisha ya raia Wa Israel ndani na nje ya nchi yao.

2. CIA. USA
Makao makuu Fairfax Virginia
Marekani ndio nchi yenye teknolojia ya hali ya juu katika mambo ya usalama kulinganisha na nchi yoyote ile. Kwa miaka mingi Idara ya ujasusi ya CIA ilikuwa ndio Idara yenye ujuzi kuliko nchi yoyote ile. Ila kwa sasa inashika nafasi ya pili. CIA ina majasusi kila kona ya dunia na imefanikiwa kupenyeza majasusi wake kila sehemu ya ulimwengu mashirika mengi ya kijasusi ya duniani huwa yana mapandizi ya CIA bila yenyewe kujua.

1. ISI PAKISTAN
Makao makuu Islamabad
Wengi inawawia vigumu kuelewa na hata kuamini Ni kwa vp nchi yenye uchumi na dhaifu na hata jeshi lililo dhaifu kiasi cha kushindwa vita Mara tatu na India kuweza kuwa namba moja katika maswala ya kiintelijensia.
Pakistan imefanikiwa mno katika maswala ya usalama kuliko nchi yoyote ile. Majasusi Wa Pakistan Ni wasiri mno kuliko wowote wale. Mafunzo kwa majasusi wapya huanza wakiwa na miaka 16 na kisha huchujwa hadi kupatikana majasusi wanaotakiwa. Intelijensia ya Pakistan ndio iliweza kumficha Osama bin Laden kwa miaka Zaidi ya 15 licha ya kwamba walijifanya wakishirikiana na CIA kumtafuta Osama.

David kagoma.

Jumatano, 21 Februari 2018

TUJIKUMBUSHE MATUMIZI YA KALAMU KWA KUFUATA RANGI

Nakuja tu na maswali chokonozi

   1. Hivi ni Kwa Nini Waalimu wanatumia kalamu ya rangi nyekundu na si bluu kama wanafunzi?
   
2. Ni Kwa Nini pia Maraisi ndio Huandikia peni nyekundu?
    Kwa nini Wakaguzi aghalabu wa Hesabu hutumia peni ya kijani?
   3. Vipi Kuhusu Kalamu Nyeusi?

nauliza hivi kwa sababu hizi rangi ukigeukia muktadha mwingine zinamaana tofauti sana mfano wengine husema unapotumia kalamu nyeusi inaa maana unatengeneza pesa na bluu maana yake unapoteza pesa ilihali nyekundu ikielekezwa zaidi kwenye mikosi

MAJADILIANO COMPILED

RANGI ZA KALAMU NA MATUMIZI YAKE .......@@!!!

Mara Nyingi sana tumekuwa tukitumia pen bila kujipa angalizo fulani hivi ama kujua mantiki yake ..................

1. Kalamu ya rangi ya Samawi/samawati (Bluu) ndiyo maarufu kutumika na wengi na hasa kwenye official document za kawaida (not mandated or authentic)
We basically have two choices when it comes to pens: black or blue. Unless you are a teacher in which case you get to use red as well........."Of course blue pens. Because they contrast better with the documents you're writing on..................The modern tradition is THAT only blue ink for all in Government.

2. Kalamu Nyeusi aghalabu hutumika kwenye miamala ya Kibiashara zaidi............."Black edges it on the grounds that it looks more professional and is a legal requirement for signing legal documents and form-filling............."Some entities are now requiring signatures in blue ink in order to differentiate the original from a copy.......Black ink is used ( where bold remarks are needed ) for business deals, display credit in a bank statement, headings etc.

3. Kalamu Nyekundu Aghalabu Hutumiwa na wenye Mamlaka Katika Kusaini Official Documents na hasa Sheria na Hati fulani fulani na mara nyingi anayeruhusiwa kutumia kalamu nyekundu ni Mh Rais na Waalimu katika kujitofautisha na wanafunzi na kuweka msisitizo zaidi kwenye masahihisho ingawa utafiti uliofanywa Marekani umewezesha kupelekea kupigwa marufuku kwa kalamu nyekundu kwa wanafunzi kutokana na wengi kutaarifu kwamba zinawatisha (psychological trauma)
http://www.dailymail.co.uk/news/article-2263874/Teachers-shouldnt-use-red-coloured-pens-mark-homework-like-shouting-upsets-pupils.html

4. Kalamu ya Chanikiwiti (KIJANI) inatakiwa kutumiwa na Wakaguzi  na hasa wa HESABU, aghalabu Peni ya kijani hutumiwa pia na Mawaziri...Majaji....ma RCs na Kamishna wa kiapo...aghalabu wataalamu wa dawa/wafamasia pia hutumia kalamu ya kijani .....Green ink is used by very senior bureaucrats as well as Ministers to sign files indicating their approval....also green color pen are used by Managers, gazetted officers, Judges and big people. Green testifies the high position and no one can question the authenticity when signed by the green color.

5. Kimsingi na KISHERIA, UNATAKIWA KILA MTU KUWA NA PENI MAALUM YA SIGNATURE. tumewahi kupata kesi ya mtu ambaye saini yake ilidukuliwa na yeye kukiri dhahiri shari kwamba ni saini yake kabisaaaa ila kwenye utetezi akasema kwamba peni iliyotumika siyo peni yake kwani ana peni maalum ya kuweka saini nyaraka zake zote za kisheria
https://keetonsonline.wordpress.com/2013/02/18/how-to-choose-the-right-pen/

6. Si salama sana kutumia kalamu nyeusi kwenye maandishi meusi, kisheria hiyo ni kopi na si halisi, jitahidi sana kutumia kalamu ya bluu kwenye maandishi meusi na hasa typed (Many copiers are so good now that black ink can look like part of a photocopy."-

7. Ball Pen ndiyo offical pen kwa nchi nyingi duniani. kumbuka Kama unatumia 'jel pen' basi ukitumia 'ball pen' mwandiko 'kitaalamu' unatofautiana (hasa kama kalamu hizo zikiwa na ukubwa wa maandishi unaotofautiana.)
"bic, speedo, cello, etc" ndio ballpoint pens.Na jell pens ni kama zile kalamu za zamani za kuchovya wino "tulikuwa tunaziita fountain - ambazo siku hizi zimeboreshwa zinawekewa wino.

8. Kuna Baadhi ya nchi;
i. mwanafunz unaruhusiwa kuandika kwa penseli na kalamu ya rangi yeyote ile (bluu, kijani, nyekundu, nk).

ii. Hawaruhusu kuweka sahihi (signature) kwa kalamu ya rangi nyingine yeyote ile isipokuwa 'bluu'. Kuna sehemu zingine hata kujaza fomu iliyochapwa ni lazima utumie kalamu ya rangi ya bluu......kalamu ya bluu ndiyo inayotambulika duniani kote (official pen)

iii. Wanatumia kalamu nyekundu kuandika jina la mtu aliyefariki (marehemu). Yaani hairuhusiwi na huwezi kuandika jina la mtu aliyehai kwa kalamu nyekundu.Mathalani ukiwa Ureno na unatumia kalamu nyekundu unahesabika ni mkaidi ama mleta mikosi ( It's considered rude to write in red ink in Portugal.)

iv: Jeshi la Marekani utatumia rangi kulingana na wadhifa (rank) wako Jeshini
In US Navy there is  a long tradition of prescribed ink colors for officers - blue color for officers, black color for departmental heads, green color for Executive officers and red color for commanding officers.

v. Huko Ujerumani, rangi ya Hudhurungi (Brown) hutumika kuweka saini HUKUMU YA KIFO ILIHALI huko Pakistan wao hutumia kalamu nyekundu kwa lengo hilohilo-Brown color ink is used to sign death warrants in Germany and red color ink was used for same purpose in Pakistan.

mfano nchi ya Australia officials pen ni NYEUSI TU! hata baadh ya benki hapa kwetu mfano NBC official pen ni nyeusi ingawa pia si salama sana kisheria .....NMB official ink ni blue,kwa documents zao....tofauti na hapo....hupokelewi.
Exim.....nyeusi na blue, CRDB.....Blue ama nyeusi; nyekundu, kwa wenye uoni hafifu na maafisa wa benki hasa kuthibitisha nyaraka

Jumanne, 20 Februari 2018

Aina za wauaji na mauaji

Hebu tujifunze jambo hapa ili tusitatizike linapotokea.. Nazungumzia kuhusu kuua.. Kutoa uhai wa mtu

1.Ameurter killers.. Wauaji wasio na ujuzi... Huacha alama huua hovyo sio wataalam.. Ni watu wanaopewa kazi wasioimudu.... Hawana shabaha... Refer tukio la TL Dom..

2. Professional killers.. Wauaji wataalam, wataaluma wanajulikana pia kama born to kill.. Yaani wamezaliwa kwa ajili ya kuua, kuangamiza.. No mistakes... No traces. Trained to assassinate...! Hawaoni shida kutoa uhai wa mtu .. Ni kama kumuua mbu....

3. Snipers.. Wadunguaji.... Hawa ni wataalam wa kutumia risasi, wana shabaha na hukaa mbali... Hawakwepeshi.. Hawakosei... Hawa nao wako kwenye kundi la born to kill ila wakiwa wamejikita kwenye sekta moja tu kudungua... Target ni moyo ama kichwa.....

4. Cold blood killers... Hawa ni watu wa kuogopwa mno.. Nadhani hawana roho wala hisia... Ni wauaji naweza kusema wenye matatizo ya akili.. Huua taratibu na kwa mateso makubwa mno.. Hawa ndio wale hutenganisha viungo kimoja baada ya kingine na sometimes kujirekodi na hata kuvipika viungo husika

5. Shooting spree killers... Hawa ni wauaji wenye msongo wa mawazo stress ama Maumivu ya mapenzi.. Hufikia kuona kila mmoja ni adui yake hivyo huchukua silaha na kutafuta kadamnasi ya watu na kuwafyatulia risasi kwa raha zake... Na mara nyingi huishia na kujimaliza na risasi ya mwisho...

6. Serial killers. Hawa ni wa mauaji ya mfululizo.. Ni wahalifu na wavunja sheria... Huanza kuua mmoja kwa sababu yoyote ile na huendelea kufanya mauaji kwa nyakati tofauti kwa sababu ile ile ama sababu nyinginezo mpaka akamatwe

7. The assassins.. Licensed to kill... Wauaji wenye vibali, leseni za kuua.. Hawa huwa ni waajiriwa wa mamlaka za nchi na huua kwa manufaa ya nchi.. Wanafundishwa kuua viongozi, wanasiasa ama mtu mwingine yeyote ambaye anaonekana ni tisho kwa usalama wa taifa, huwa hawashtakiwi popote ... Sometimes hutumika vibaya na mamlaka...!!!

8. The hangers... Wanyongaji hawa ni watu wema wenye ajira rasmi... Kazi yao ni kuwanyonga wahalifu wote waliohukumiwa hukumu ya kifo.. Hawa hufanya ibada pamoja na watu wanaotarajia kuwanyonga.

Na David kagoma.

Jumamosi, 17 Februari 2018

Espionage & Diplomatic Blunder: KGB walipompa balozi wa Marekani zawadi iliyofichwa kifaa cha kunasia sauti (BUG)

Mnamo mwaka 1946, kundi dogo la wanafunzi watoto wa shule wa nchini Urusi kutoka katika kikundi kidogo kilichojulikana kama "Vladimir Lenin All-Union Pioneer Organization (wapo kama vijana flani hivi wa skauti wa hapa Bongo) walimpatia zawadi ya nembo ya taifa la marekani (kama huku kwetu Tanzania ni ile nembo yetu ya bibi na bwana) ndugu Avarell Harriman, aliyepata kuwa balozi wa Marekani nchini Urusi (USSR)

Ile zawadi, kama ishara ya urafiki mwema wa urusi kwa marekani ambaye alikuwa ni mshirika wake mkuu katika vita ya pili ya dunia, ilikuja kuning'inizwa katika eneo maalum la makazi ya balozi huyo yaliyokuwapo katika jiji kuu la Moscow.

Nembo ile ya taifa la marekani iliendelea kuning'inia pale ukutani kwa kwenye makazi ya balozi kwa muda wa miaka saba (7), mpaka kwa bahati mbaya wataalam kutoka wizara ya mambo ya nje (bila shaka ni maofisa wa CIA) walipokuja kugundua kumbe ile zawadi ilikuwa ni zaidi ya urembo wa ukutani.

Mara paaaaaap, kumbe ilikuwa ni kifaa cha kunasia mazungumzo (bugging device)........!!!!!

Warusi waliunda kifaa cha kusikilizia mazungumzo kwa siri sana (bug), ambacho makachero wa kupambana na wapelelezi wa nchi hasimu (counterintelligence unit) wa Marekani walikitunga jina na kukiita (The Thing).

Kifaa kile kilifichwa kwa usiri sana ndani ya nembo ya taifa la Marekani na kimekuwa kikisikiliza mazungumzo ya balozi Harriman pamoja na mabalozi wote waliomfuata kwa kipindi chote ambacho kifaa kile kilikuwa kinaning'inia mule ndani.

Balozi yule alikiri kwa kusema ya kuwa Ilidhihirisha siku ile kumbe USSR ilikuwa na wataalam wa kutisha sana wa masuala ya electronics.

Balozi alisema ya kuwa sasa ninaamini ya kwamba kwa ugunduzi huu utaalam mzima wa serikali kusikilizana siri umefikia viwango vya hali ya juu sana vya technology.

Wanadiplomasia pamoja na wamarekani wengine waliokuwa wakifanya kazi katika ubalozi wao pale USSR walikwisha amini zamani hata kabla ya kuwa kuta zote zilizopo jiji la Moscow "zina masikio"

Aliyewahi kuwa rais wa marekani kwa miaka ya zamani sana bwana James Buchanan aliwahi kisema ya kwamba mara zote wanadiplomasia wetu huzungukwa na mashushushu wenye taaluma zote kubwa na ndogo, na ni mara chache sana tunaweza kukodisha ama kuajiri mtumishi wa ndani ambaye sio informer wa polisi.

Mwanzoni mwa karne ya 20, ujasusi kwa njia za kibinadamu pamoja na usikilizaji wa mazungumzo ulijawa na technology mpya ya nyaja pamoja na vifaa vidogo vya kusikilizia na kurekodia mazungumzo.

Wageni wote waliokuwa wakiingia katika nyumba ya makazi ya balozi walikuwa wakipewa kadi punde tu wanapowasili wakitahadharishwa ya kuwa nyumba vyote pamoja na bustani ndani ya eneo lile vilikuwa vinapelelezwa kwa ukaribu sana na makachero wa KGB.

Hiki kifaa kiliundwa na bwana Termen, ambaye alipata kuishi nchini Marekani kwa kipindi kirefu kidogo kisha akaja kurudi Urusi kabla ya vita ya pili ya dunia.

Baada ya kuwasili Russia, bwana theremin alipelekwa moja kwa moja katika chuo cha siri chenye maabara kisha kupewa jukumu la kuunda na kuja na njia ya kitaalam ya namna na kusikilizia mazungumzo ya nyumbani kwa balozi wa Marekani nchini Russia.

Kifaa alichofanikiwa kuunda mtaalamu huyo kilikuwa na antenna pamoja na cylinder pamoja na waya mdogo sana uliotumika kama microphone. Majasusi wa KGB waliokuwa wanazurura maeneo ya mtaa huo ambapo kuna makazi ya balozi wa marekani, walikuwa na uwezo wa kuwasha hicho kifaa kwa remote maalum inayotumia mawimbi ya radio.

Sasa pale ambapo balozi ama mtu mwingine yeyote aliyepo chumbani akiongea, yale mawimbi ya sauti yalikuwa nayawaendea moja kwa moja vijana wa KGB na kuweza kusikiliza mazungumzo mazima.

Maajabu ya hicho kifaa ni katika udogo wake. Kilikuwa ni kidogo mno. Tena saaaanaa aiseee. Kilikuwa hakitumii chanzo chochote cha umeme wali betri, hakukuwa na nyaya ambazo zingeweza kugundulika wala betri za kubadilisha na kiliweza kifanya kazi pindi tu KGB wakikiwasha kwa remote inayotumia mawimbi ya redio. Laa sivyo kinazimika kiasi kwamba wakaguzi wa CIA wasingeweza kukigundua.

Wizara ya mambo ya nje ya marekani kupitia wataalam wake wa kufagia vifaa vya kunasia sauti (bug sweepers) walipatwa na mashaka kwamba KGB waliunda kifaa cha namna hii pale ambapo wataalam wa mawimbi ya radio kutoka jeshi la marekani pamoja na uingereza waliokuwa wanachungua mawasiliano ya USSR bila kutarajia wakajikuta wanakamata mawasiliano ya sauti ya wanadiplomasia wao kwa kutumia vifaa vyao wenyewe.

Matukio ya namna hiyo pamoja na kitendo cha marekani kuruhusu wafanyakazi wa urusi kufanyia marekebisho nyumba ya balozi wao kabla ya kuhamia mwaka 1952, ambapo ndio ili nafasi nzuri kwa KGB kupandikiza vifaa vya kusikilizia, ilipelekea CIA kutuma wataalam wake kupitia wizara ya mambo ya nje kwenda kufagia nyumba nzima (bug sweeping) bila mafanikio.

Walitoka kapa mpaka wakaanza kushuku labda KGB wamebadili mbinu zao za kupandiliza vifaa ama taaluma ya CIA ya kugundua vifaa hivyo ndio imepitwa na wakati.....!!!!!

Baada ya kuona hali si hali, wizara ikaamua kutuma tena wataalam wawili, Ford pamoja na Bezjian, mpaka Moscow kufanya zoezi upya tena kwa kina na umakini zaidi. Bezjian akahisi labda KGB waliondoa kifaa chao kabla zoezi jipya la ukaguzi halijaanza na kisha kupachika tena hali ilipokuwa shwari.

Ili kuwakamata vizuri KGB, akaamua kujifanya kama tu ni mgeni wa balozi Kennan. Vifaa vyake vya kazi vilikuwa vipo tayari na vimefichwa vizuri kabisa hata kabla hajafika na kisha kukaa pale kwa balozi kwa siku kadhaa huku akicheza karata na kuwaangalia kwa umakini wafanyakazi wa nyumba ya balozi wakati huo anatumia muda wa usiku kutafuta kifaa hicho cha kunasia sauti. Lakini safari hii wakachemka tena. Hola. Wakatoka patupu.

Sasa jioni moja wakati balozi yupo kwenye chumba chake hicho akiwa anasoma kwa sauti ya chini kidogo baadhi ya nyaraka zake za siri wakati wataalam wa CIA bwana Ford na Bezjian wakiwa wanazunguka nje ya nyumba wakiwa na vifaa vyao vya detection, ghafla Bezjian akafanikiwa kukamata sauti ya bwana Kennan kwenye receiver yake na kisha taratiiibu kabisa akaamua kuifuatilia ile signal mpaka chanzo chake inapotokea.

Bezjian akaenda katika chumba cha kusomea na kumwambia Kennan kwa ishara kwa aendelee kusoma kwa sauti zaidi kwa maana kuna signal ameikamata. Ile signal iliyokuwa na sauti ya Kennan ilionekana inatokea katika kuta nyuma ya ile "zawadi aliyopewa balozi.

Bezjian akaondoa ile zawadi kutoka ukutani kisha kwa kutumia nyundo akaanza kupasua ukuta ambapo ile zawadi ilikuwa imetundikwa. Wakati anabomoa ukuta signal ikapotea ghafla.

Bezjian ndipo machale yakamcheza kuwa kile kifaa cha sauti hakikuwa katika ukuta, bali kilikuwa ndani ya ile zawadi ya balozi na kisha kuamua kuvunja ile zawadi kwa kutumia nyundo ile ile.

Ndani ya dakika chache zoezi likakamilika na yule mtaalam wa CIA akakuta ndani ya ile zawadi kulikuwa na kifaa kidogo sana kinachoweza kulingana na penseli.

Kwa usiku wote ule, ofisa wa CIA bwana Bezjian akaamua kulala na kifaa kile chini ya mto wake ili kwamba KGB wasije kukiiba. Kesho yake kifaa kikapelekwa kwenda marekani chaaaaap ili kisomwe na kitengenezwa mbadala wake na idara za usalama za marekani jambo ambalo likawa kama vile ndio chanzo cha mashindano ya silaha baina ya USSR na USA katika kuunda vifaa vya kunasa mawasiliano vya hali ya juu zaidi ili kila mmoja amchunguze mwenzake zaidi.

Kwa miaka mingi sana hii zawadi ya mtego ilining'inizwa juu ya kuta za nyumba ya balozi wa marekani iliyokuwa busy sana na wageni wa aina tofauti tofauti mpaka wale wa levels za juu sana kama General wa jeshi Eisenhower, watumishi wa ikulu ya marekani pamoja na wabunge wengi sana, wakibadilishana taarifa mbali mbali kuhusiana na hali ya usalama na ustawi wa nchi yao.

Mmoja wa watumishi wa KGB ambaye alikuwa anasimamia kifaa kile akaja kukiri baadaye ya kuwa kile kifaa kiliwawezesha kupata taarifa muhimu zilizowezesha USSR kuweza kuwazidi kete wamarekani katika siasa za dunia wakati wa kipindi kigumu cha vita baridi.

*****MWISHO WA MAKALA*****
==========================