Jumamosi, 3 Machi 2018

USHAHIDI: "VICARIUS FILII DEI" NI 666.
_
Wakatoliki wamekuwa wakipinga mara nyingi kwamba Vicarius Filii Dei sio jina la papa na wala haina hesabu ya 666. Ukurasa mmoja wa Facebook wa majeshuiti unaoitwa "Asali Itokayo Mwambani" umejaribu kupotosha watu kwamba Vicarius Filii Dei kamwe sio jina la papa, na haifiki 666 kwa kuwa "u" haiwezi kugeuzwa na kuwa "v"! Hii hapa ni njia nyepesi ya kufunua uongo huu wa kijeshuiti. Tutazingatia Mambo mawili yafuatayo.
,
MOJA: Je "u" haiwezi kuwa "v" katika kilatini?
,
?Hii ni njia moja ambayo hawa majeshuiti wa katoliki wanaitumia kusema kuwa Vicarius Filii Dei haiwezi kuwa 666 kwa kuwa "u" huwezi kuigeuza na kuwa "v"! SASA nadhani kwa muda huu ungewapa hawa majeshuiti "A" au hata ungewapa "100%" kwamba wako sawa! Lakini kabla hujawapa hiyo "A", tafadhari tafuta dokomenti au sarafu za mapapa kisha uone herufi "u" ambavyo katika kilatini imeandikwa kama "v"; nitakusaidia kwa kukupa mifano halisi michache ifuatayo ambayo itaziba kabisa midomo yao.
,
a. Jina la papa "Pius" XI, limeandikwa kama "Pivs" kwenye medari yake ya mwaka 1929 iliyotolewa kwa ajili ya mkatabwa wa Lateran (angalia picha:  https://sabbathlight.files.wordpress.com/2017/11/1929.jpg).
,
b. Jina la papa "Paulus" VII, limeandikwa kama "Pavlvs" kwenye sarafu 100 Lire ya Vaticano ya mwaka 1963 (angalia picha: (https://sabbathlight.files.wordpress.com/2017/11/1963.jpg).
,
Hivyo utaona wazi jinsi gani Wakatoliki wanajifunua wenyewe kwamba "u" pia ni "v". Na kama ukichukua "Vicarius Filii Dei" na kuigeuza kuwa "Vicarivs Filii Dei" utapata 666:
V. . . . . .5
I. . . . . . 1
C. . . . . .100
A. . . . . .0
R. . . . . .0
I. . . . . . .1
V. . . . . . 5
S. . . . . . 0
= . . . . . 112
_
F. . . . . . .0
I. . . . . . . 1
L. . . . . . .50
I. . . . . . . .1
I. . . . . . . .1
=. . . . . . .53
_
D. . . . . .500
E. . . . . . . 0
I. . . . . . . .1
=. . . . . . 501
_
VICARIVS = 112
FILII        =   53
DEI          =  501
Jumla      =  666.
#  #  #  #  #  #  #  #  #  #  #  #  #  #
MBILI: Je VICARIVS FILII DEI sio jina la papa?
,
HUU ni uongo mwingine ambao wakatoliki huutumia kukataa namba 666 kwamba haimhusu papa. Wanasema papa kamwe hajawahi kutumia, na wala hata sasa hatumii jina hilo la Vicarivs Filii Dei. Hii ni njia nyingine ambayo makuhani na viongozi wa katoliki huitumia kuwaliwaza makundi yao ili kamwe wasije kuona ukweli. VICARIVS FILII DEI ni jina la papa na kuna maelfu ya ushahidi wa jina hilo kutoka kwa dokomenti za wakatoliki wenyewe. Hapo chini tutaangalia dokomenti chache katika hizo. (Msisitizo wa kwangu).
_
Gazeti la katoliki la "Our Sunday Vistors" katika mwaka 1914 liliandika kwamba:
,
“Jina la Papa katika Roma ni Vicarius Filii Dei. Jina hili limeandikwa kwenye kilemba chake[*]; na kama ukizichukua herufi za jina lake ambazo zinawakisha namba za Kilatini na kuzijumlisha kwa pamoja zinaleta 666.” —(Our Sunday Visitor, (Gazeti la Katoliki la kila wiki), November 15, 1914, chini ya ‘Bureau of Information’, p. 3)). [angalia nakala ya gazeti hili hapa: http://remnantofgod.org/osv1914.htm)
,
Mwaka uliofuata, ambao ni mwaka 1915 gazeti lilelile la Our Sunday Vistor likaandika tena kwamba:
,
"Maneno yaliyoandikwa katika kilemba cha Papa ni haya VICARIUS FILII DEI ambayo ni ya kilatini kwa ajili ya ‘KASISI WA MWANA WA MUNGU’. Wakatoliki huchukulia kwamba kanisa ambalo ni jumuiya ya kuonekana, lazima liwe na kichwa cha kuonekana. . . Maadui wa Upapa hukanusha jina hili kama dhana mbaya lakini Biblia inatuambia kwamba Kristo hakuwapa Kanisa lake mamlaka ya kufundisha tu, bali pia mamlaka ya kutawala. Kudai kuwa na mamlaka ya kutawala katika ufalme wa Kristo wa kiroho, katika nafasi ya Kristo , sio madhara zaidi kuliko kudai kuwa na mamlaka ya kufundisha kwa jina la Kristo.” —(Our Sunday Visitor, (Gazeti la Katoliki la kila wiki), April 18, 1915, swali la 30 chini ya ‘Bureau of Information’, p. 3)). [angalia nakala ya gazeti hili hapa: http://remnantofgod.org/osv1915.htm]
,
Tangu ukweli wa 666 ujulikane, mapapa walisimama kulitumia jina la Vicarius Filii Dei kwa wazi, ili kuwadanganya wakatoliki kwamba sio jina la papa, lakini dokomenti zao zenyewe zinawafunua. Kadinali Manning anasema:
,
"Ilikuwa ni utii wa heshima kusujududu kwa KASISI WA MWANA WA MUNGU, na kusuluhisha usuluhisho wa malalamiko yao kwa mtu ambaye wote wangekubali kutii.” —(The Temporal Power of the Vicar of Jesus Christ, pp. 231-232 na Henry Edward Kadinali Manning, toleo la pili, London: Burns and Lambert, 1862).
,
Kasisi wa Mwana wa Mungu = Vicarius Filii Dei.
,
Angalia Dokomenti za kilatini zifuatazo kutoka kanisa katoliki, ambazo kwa wazi zinatumia jina Vicarius Filii Dei. Moja inatoka kwenye kitabu kinachoitwa "Prompta Bibliotheca" kilichoandikwa na Lucius Ferraris; ambacho Insaiklopedia ya Ukatoliki inasema kimejaa maelezo ya thamani:
,
“Ut sicut Beatus Petrus in terris VICARIUS FILII DEI fuit constitutus, ita et Pontifices eius successores in terris principatus potestatem amplius, quam terrenae imperialis nostrae seremitatis mansuetudo habere videtur.” —(Prompta Bibliotheca Canonica, Juridica, Moralis, Theologica, Ascetica, Polemica, Rubristica, Historica, by Lucius Ferraris, Volume V, makala ya “Papa, Article II”, yenye kichwa “Concerning the extent of Papal dignity, authority, or dominion and infallibility”, point #20, column 1828, ilichapishwa katika Petit-Montrouge (Paris) na J. P. Migne, toleo la 1858)). [angalia dokomenti yenyewe hapa: http://www.lightministries.com/id788.htm]
,
Ikitafsiriwa kwa kiswahili dokomenti hii inasomeka: “Kama vile Petro mbarikiwa alivyofanyika KASISI WA MWANA WA MUNGU duniani, kwa hiyo inaonekana kwamba maaskofu wakuu, waandamizi wake, wanashikilia kutoka kwetu na ufalme wetu nguvu ya ukuu duniani ya juu kuliko uzuri wa utulivu wetu wa kifalme duniani.”
,
Dokomenti nyingine ya kilatini inayotumia jina hilo inasema:
,
“Beatus Petrus in terris VICARIUS FILII DEI videtur esse constitutus.” —(Decretum Gratiani, prima pars, dist. xcvi, col. 472, (kwanza ilichapishwa katika Bologna mwaka 1148, na ikachapwa tena mwaka 1555)). Dokomenti hii ilitafsiriwa katika kiingereza na Christopher B. Coleman, Ph. D., katika kitabu kinachoitwa “The Treatise of Lorenzo Vallo on the Donation of Constantine,” p. 13. New Haven: Yale University Press, 1922.
,
Ikitafsiriwa katika kiswahili nukuu hiyo ya juu inasomeka: “Petro mbarikiwa anaonekana kuwa amefanyika KASISI WA MWANA WA MUNGU duniani.”
,
Nukuu mbili za kilatini zifuatazo zote zina maana ileile kama ya moja hapo juu, na zote zinatumia jina la Vicarius Filii Dei,, Ya kwanza inasema:
_
“Beatus Petrus in terris VICARIUS FILII DEI esse videtur constitutus.” —(Corpus Juris Canonici, Gregorii XIII, Pontif. Max., Auctoritate, Distinctio 96, Column 286, Canon Constantinus 14, Magdeburg, 1747.
Jina alilopewa Papa ni “Vicarius Filii Dei.” Sacrosancta concilia ad regitionem exacta, na Philippe Labbe, SJ., Vol. I, p 1534: Paris, 1671).
,
Nukuu hiyo hiyo tena, lakini inatoka kwenye kitabu kingine tofauti inasema:
,
“Beatus Petrus in terris VICARIUS FILII DEI esse videtur constitutus.” —(Corpus Juris Canonici Emendatum et Notis Illustratum Gregorii XIII. Pont. Max., Lvgdvn., MDCXXII, col. 295).
,
Ni mkatoliki pekee ambaye aidha ana kichwa kigumu au moyo mgumu ndiye atakataa ushahidi wote huu, na kupinga kwamba VICARIUS FILII DEI--666--sio jina la papa. Ukweli ni kwamba kuna maelfu ya dokomenti za katoliki zinazokili kwamba Vicarius Filii Dei ni jina la papa! Lakini hatutaki kukuchosha kwa kusoma maneno mengi. Tunaamini kwa haya machache utachukua hatua ya kuchunguza na kuhakikisha wewe mwenyewe. Na tunaomba ufanye hivyo kwa Jina la Yesu Kristo.

Maoni 1 :

  1. Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

    Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

    Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

    Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

    Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159

    JibuFuta