Jumanne, 11 Julai 2017

Haikuwa Kazi rahisi Ukristo ukatoliki kukufikia hadi wewe huko kijijini kwenu!!! Kwa kifupi ngoja nikupe jinsi watu 12 (Mitume) walivyochanja maziwa, mito, mabahari, majangwa, misitu, mabonde, milima na tambarare hadi kukufikia wewe!!!
Na usijisifu kwa kuwa u ndani ya Kanisa Moja, Takatifu, Katoliki la Mitume; ni KWA NEEMA YA MUNGU TU ndugu yangu!

Ilikuwaje basi!!!!?

Baada ya Pentecoste, mitume walibaki Palestina "kwa muda mfupi" na baadaye kidogo, pole pole, wakaanza kusambaa sehemu mbali mbali za "dunia" hasa baada ya kifo cha kifiadini cha Stephano (kama Mwaka 34 B.K) na cha Yakobo (43 B.K).

PETRO: mvuvi mwenyeji wa Bethsaida, baada ya kukaa Palestina kwa muda, alikwenda SYRIA na ASIA NDOGO (Asia Minor). Alikuwa Askofu wa Antiokia tangu 37-53 B.K). Baadaye alikwenda Roma ambako alisulibishwa kichwa chini miguu juu mwaka 67 akiwa na umri wapata miaka 70. Ni Msimamizi na muombezi wa Wavuvi na Utawala wa Papa (Papacy).

ANDREA: Mdogo wa Petro, vile vile mvuvi kutoka Bethsaida. Alikwenda kuhubiri Asia Ndogo, SCYTHIA, na mwishowe UGIRIKI. Aliuawa kwa kusulibishwa Mwaka 69 B.K akikisiwa kuwa na miaka 65. Ni mwombezi na msimamizi wa wavuvi.

SIMONI: Mzeloti, alikwenda kuinjilisha MISRI, AFRIKA YA KASKAZINI, BRITANIA (BRITAIN) na IRAN. Alikufa kwa kwa "kuatiliwa" (kukatwa katwa mwili), yaani Mutilation akikadiriwa kuwa na miaka 70's. Ni muombezi na msimamizi wa "curriers".

YUDA (Thaddeus): aliondoka Palestina na kwenda OSROENE, ARMENIA na IRAN. Alikufa Mwaka 79, inasemekana kwa kuteswa (impalement) akikadiriwa kuwa na miaka 70's. Ni muombezi na msimamizi wa mambo magumu na hali zenye kukatisha tamaa (hopeless cases and desperate situations).

THOMASI: alitoka Palestina akaelekea ORSOENE, ARMENIA, MISRI na mwishowe INDIA na BURMA. Alikufa kwa kuchomwa kisu/visu (stabbed to death) Mwaka 72 ikiaminika akiwa kwenye miaka 60's. Inaaminika kuwa alikuwa mseremala (carpenter) na ni muombezi na msimamizi wa wasanifu majengo (architects) na wakandarasi (construction workers).

MATHAYO (Mtoza ushuru). Alikaa kwanza Palestina na, labda, baadae alikwenda MISRI na ETHIOPIA na mwishowe IRAN. Alikufa kifo cha kawaida (natural death) Mwaka 90 akisadikiwa kuwa na umri wa miaka 90. Aliandika Injili yake kabla ya Mwaka 70. Ni msimamizi wa wahasibu, mabenki, walinzi, watunza kumbukumbu, watoza ushuru na custom agents.

YAKOBO (Mdogo, the less): alibaki Palestina maisha yake yote kuwainjilisha Wayahudi. Aliuawa kwa kupigwa mawe Mwaka 62 akikisiwa kuwa na umri wa miaka 60.

YAKOBO (mkuu, the great): kaka wa Yohane na binamu "cousin" wa Yesu (mama zao ni ndugu). Huyu ndiye mtume wa kwanza kufa, alikatwa kichwa Mwaka 43 akiwa ktk umri wa mwanzo mwanzo wa miaka 40 (early 40's). "Ni kama" alienda HISPANIA na akarudi kuwa askofu wa YERUSALEM. Ni msimamizi wa Wahujaji, Wafamasia, Wagonjwa wa homa ya baridi yabisi (Arthritis) na Rheumatism.

YOHANE: Mdogo wa Yakobo, wavuvi wazaliwa wa Bethsaida. Huyu ndiye mtume aliyeishi miaka mingi kuliko wote. Alifia EFESO baada ya kufanya utume PALESTINA, ROMA na ASIA NDOGO. Alimtunza Mama wa Yesu hadi mama huyo alipofariki. Aliandika Injili ya nne (fourth gospel), barua tatu na Kitabu cha Ufunuo ktk kisiwa cha Patmos Mwaka 97. Alikufa Mwaka 100 akiwa na miaka 97. Ni msimamizi wa Wahariri, Wachapishaji maandishi na Urafiki.

FILIPO: vile vile mvuvi toka Bethsaida, alitoka Palestina baada ya kifo cha Yakobo Mwaka 43, akaenda AFRIKA YA KASKAZINI na ASIA NDOGO. Alikufa kwa kusulibishwa Mwaka 90 akiwa na miaka 87.

BATOLOMAYO (NATHANAEL): alikuwa anatokea Kana (Galilaya) na alikuwa mvuvi pia! Alifanya utume wake PALESTINA, ASIA NDOGO, ARMENIA na INDIA YA KATI (Central India). Alikufa Mwaka 63 kwa kuchunwa ngozi (flay) na kusulibiwa ikiaminika akiwa na miaka 57. Ni msimamizi wa watega wanyama au wawindaji (trappers).

Nimeona niwashirikishe labda yaweza kuwa msaada kwa mmoja au watatu hapa!

Nimetafsiri kutoka pamphlet "The Spiritual Legacy of the Catholic Church" by Robert Haas. pp 3-4.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni