IJUE SALA YA SALAM MARIA MJUE BIKIRA NA ROSARY
Rosary ni jina la kilatini ambalo lina maana ya bustani ya maua ya waridi
Neno rosary limetokana na neno ROSE ambalo kwa lugha ya kiingereza linaaanisha ua la waridi.Ua waridi ni ua la inalopendwa sana na kujulikana sana kuliko maua yote unaposali sala ya rosary unafanana na mtu aliyeingia katika bustani ya maua waridi na kuyachuma kisha kutengeneza shada au taji la maua hayo kisha kumkabidhi Mama yetu Bikira Maria azikabizi sala zako kwa Mungu kama zawadi ndiyo maana katika litania ya loreto huwa tunamwita Bikira Maria kwa jina la waridi lenye fumbo au Rosa Mystica
#Je sala ya rosary inauhusiano wowote na biblia takatifu?
Sala ya rosary takatifu husaliwa kwa kurudia rudia sala ya salamu maria mara 10 kwa kila fumbo pamoja na kusali sala ya baba yetu mara moja kwa kila tendo kwa matendo yote matano mbaka yaishe huku ikitanguliwa na kanuni ya imani
Hivyo asilimia kubwa ya sala ya rosary imetengenezwa ana sala ya salamu maria pamoja na sala ya baba yetu
Hivyo tukitaka kujua uhusiano kati ya sala ya rosary na biblia takatifu inatupasa kwanza kujua uhusino kati ya sala ya salamu maria na biblia takatifu pamoja na uhusiano wa sala ya baba yetu na biblia takatifu
#Je sala ya salamu maria imetoka kwenye biblia
Sala ya Salamu Maria imetoka kwenye biblia takatifu kwa kuunganisha vifungu mbalimbali vya biblia takatifu vinavyopatikana katika injili ya luka kama ifuatavyo
#salamu maria umejaa neema bwana yu nawe (luka1;26-28)
(luka1;26-28)
“ mwezi wa sita malaika Gabrieli alitumwa kwenda mji wa galilaya jina lake Nazareti kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu jina lake Yusufu wa mbali ya Daudi na jina lake bikira huyo ni Marium akaingia nyumbani mwake akasema salamu uliyepewa neema bwana yu nawe”
Maneno hayo yanatoka kutoka katika injili ya luka pale malaika gabrieli anapomtaarifu bikira maria kwamba atapata mimba kumzaa bwana wetu Yesu Kristu
#umebarikiwa kuliko wanawake wote naye Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa
Luka 1;41-43 “Ikawa Elizabeth aliposikia kule kuamkia kwake Mariam kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake ,Elizabeth akajazwa roho mtakatifu akapaza sauti akasema umebarikiwa wewe katika wanawake naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa”
Kwa kuwa Elizabeth aliyasema hayo baada ya kujazwa na roho mtakatifu basi ni dhahiri kuwa Mungu mwenyewe ameyathibitisha hayo kupitia kwake
Maneno hayo aliyasema Elizabeth alipojazwa na roho mtakatifu baaba ya kutembelewa na bikira maria .hivyo tunaweza kuseema ni Mungu Roho mtakatifu mwenyewe aliyeyathibitisha hayo
#Maria mtakatifu Mama wa Mungu(luka1;43)
luka 1;43
Elizabeth akajazwa roho mtakatifu akasema umebarikiwa wewe katika wanawake ,naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?
Nb. neno bwana lilikuwa likitumika kumaaanisha Mungu kwa wakati ule
Hivyo ni sawa na kusema kuwa Elizabethi alisema limenitokeaje neno hili hata mama wa Mungu wangu anijilie mimi
# Utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu amina
Hapa ndipo pale sisi tunapotaja maombi yetu kwamba atuombee kwa Mungu hasa saa yetu ya kufa kwa kuwa ni wakati wa kufa ndipo mtu anapohitaji sana msaada wa maombezi kwa kuwa yey ne mwenyewe anakua hana nguvu za kujiombea
Vifungu hivyo hapo juu ndivyo vinavyotupatia sala nzima ya salamu Maria ambayo imetokana na kuviunganisha pamoja vifungu hivyo na kutuletea sala nzima ambayo ni
“Salamu maria umejaa neema bwana yu nawe umebarikiwa kuliko wanawake wote naye yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa maria mtakatifu mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu amina “
Jambo zuri ni kwamba kila mara unapoisali sala hii ni sawa na kurudia maneno aliyoyatamka malaika Gabriel alipokuwa ananampasha habari maria kwamba atakuwa mama wa mungu pamoja na ukweli aliouthibitisha mungu roho mtakatifu kupitia kwa Elizabeth hivyo kuifanya sala hiii ya salamu maria kuwa na nguvu mbele za mungu katika maombi yetu
Unashindwaje kumheshimu bikira maria wakati malaika Gabriel mwenyewe alikuwa wa kwanza kumheshimu ! hakika wanakosa mengi wale wasiojua kumheshimu mama wa mkombozi kwani kuna neema na Baraka za pekee kupitia msaada wa maombezi yake
# je sala ya baba yetu inapatikana wapi
Wengi tunafahamu tu kuhusiana na sala ya baba yetu ambayo inapatikana sehemu mbalimbali katika injili pale Yesu alipokuwa akiwafundisha wanafunzi wake namana ya kusali sala hii tunaweza kuipata vizuri katika injili ya Mathayo 6;9-13
Basi ninyi saline hivi baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe ufalme wako uje mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama mbinguni utupe leo riziki zetu kama sisi nasi tuwasameavyo wadeni wetu na usitutie majaribuni lakini utuokoe na yule mwovu
Hivyo kwa kuangalia asili ya sala ya salamu Maria na sala ya baba yetu ,kwamba zote zimepatikana katika vifungu kadhaa kutoka katika biblia takatifu ni wazi kwamba sala zima ya rosary takatifu asili yake ni kutoka kwenye biblia takatifu kwani inaundwa na sala hizo mbili na Zaidi tunaisali kwa kuzirudia sala hizo mara kadhaa
Pia nguvu ya sala hii kwenye imani inapatikana katika mafungu yake ya rosary ambayo yanasaliwa kwa kutafakali hatua Fulani ya ukombozi wa mwanadamu yaani kutafakari nyakati kadhaa alizopitia bwana wetu Yesu kristu iwe katika kipindi cha furaha (matendo ya furaha) iwe kipindi cha tabu (matendo ya uchungu) iwe kipindi cha shangwe (utukufu) .hivyo kukamilisha maisha yote anayoweza kuyaishi mwanadamu hapa dunia kwa kuwa neno alijifanya mtu kwa kutupenda sisi
# je bikira Maria ni mtakatifu?
Jibu la swali hili linapatiakana katika kitabu cha injili ya luka (1;46-48)
“Mariamu akasema moyo wangu wamwadhimisha bwana na roho yangu imemfurahia mungu mwokozi wangu kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi wake kwa maana tazama tokea sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa”
Maneno hayo aliyoyasema maria yanathibitisha waziwazi kwamba bikira maria mwenyewe akiongozwa na Mungu alitabiri heshima yake ya kuheshimiwa na vizazi vyote ..yaaani kwamba vizazi vyote tokea wakati ule hadi kizazi chetu tutamheshimu yeye yeye kama mbarikiwa ama mwenye heri
#je bikira Maria amejaliwa neema nyingi?
(luka1;26-28)
“mwezi wa sita malaika Gabrieli alitumwa kwnda mji wa Galilaya jina lake nazareti kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu jina lake yusuphu wa mbali ya Daudi na jina lake bikira huyo ni marium akaingia nyumbani mwake akasema salamu uliyepewa neema bwana yu nawe”
Hivyo malaika Gabriel mwenyewe anathibitisha kuwa bikira Maria amepewa neema/amejaliwa neema
# je Bikira Maria ni mama wa Mungu?
Jibu la swali hili linapatikana katika kitabu injili ya luka 1;43
“Elizabeth akajazwa Roho mtakatifu akasema umebarikiwa wewe katika wanawake ,naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.limenitokeaje neon hili hata mama wa bwana wangu anijilie mimi? “
Nb. neno bwana lilikuwa likitumika kumaaanisha Mungu kwa wakati ule
Hivyo ni sawa na kusema kuwa Elizabethi alisema limenitokeaje neno hili hata mama wa Mungu wangu anijilie mimi
Tena ikumbukwe kuwa maneno hayo aliyasema huku akiwa ameongozwa na Roho mtakatifu, hivyo ni kwamba ni Mungu mwenyewe ndiye anatufunulia hayo kupitia Elizabeth
# je Bikira Maria amebarikiwa kuliko wanawake wote?
Jibu la swali hili linapatikana katika kitabu cha luka 1;41-43
” Ikawa Elizabeth aliposikia kule kuamkia kwake Mariam kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake ,Elizabeth akajazwa roho mtakatifu akapaza sauti akasema umebarikiwa wewe katika wanawake naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa”
Kwa kuwa Elizabeth aliyasema hayo baada ya kujazwa na roho mtakatifu basi ni dhahiri kuwa Mungu mwenyewe ameyathibitisha hayo kupitia kwake
#je Bikira Maria ni mama yetu pia?
Jibu la swali hili linapatikana katika kitabu cha injili ya yohana 19;25-27 pale Yesu alipokuwa anakaribia kufa alitukabidhi sisi sote kwa mam Bikira Maria kupitia kwa Yohana
Yohana19;25-27
”Na penye msalaba wake Yesu walikuwepo wamesimama mamaye (Bikira Maria) na umbu la mamaye Mariam wa klopa ana mariamu Magdalena, basi yesu alipomuona mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda(yohana)amesimama karibu alimwambia mama yake mama tazama mwanao kisha akamwambia yule mwanafunzi tazama mama yako na tangu saa ile yule mwanafunzi akamchukua nyumbani kwake”
Hivyo kupitia kumkabidhi Bikira Maria kwa yohana kama mama yake pale aliposema kuwa mtazazme mama yako anathibitisha kwamba hata sisi sote tunaweza tukamwita bikira maria kwa heshima kama mama yetu
Pia kupitia maneno ya Yesu aliyomwambia mama yake(Bikira Maria) kwamba mtazame mwanao alikuwa akimaanisha kwamba sisi sote ni watoto wa mama Maria
#kwanini Yesu alimkabidhi Bikira Maria kwa mtume Yohana?
Biblia takatifu haijaelezea kifo cha mtakatifu Yosefu wala haijaelezea alikufa lini lakini inasadikika kuwa baada ya kuzaliwa Yesu Bikira Maria hakuishi na mtakatifu Yosefu kwa muda mrefu ndiyo maana baada ya kuzaliwa Yesu huwezi kusikia tena habari za Yosefu tena kwa uthibitisho Zaidi rejea injili ya yohana wakati Yesu anakufa msalabani ,aliamua kumkabidhi mama yake kwa mtakatifu Yohana ,
Yohana19;25-27
”Na penye msalaba wake Yesu walikuwepo wamesimama mamaye (Bikira Maria) na umbu la mamaye Mariam wa klopa ana mariamu Magdalena, basi yesu alipomuona mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda(yohana)amesimama karibu alimwambia mama yake mama tazama mwanao kisha akamwambia yule mwanafunzi tazama mama yako na tangu saa ile yule mwanafunzi akamchukua nyumbani kwake”
Tena tunaambiwa kuwa yohana alimchukua mama yake Yesu akaenda kuishi na kumtunza nyumbani kwake .
Hii inamaanisha nini?
Hiii inamaanisha kwamba Yosefu hakuwa hai hadi wakati wa kifo cha Yesu ..kwamba alikufa mapema hata kabla Yesu hajaianza kazi yake ……Labda ndiyo mpango wa mungu kwamba Maria abaki bikira daima! Kwani tunaambiwa kwamba Yosefu hakumjua Maria kamwe hata baada ya kumzaa Yesu
Kuzidi kujua Zaidi ukweli kuhusu kifo cha mtakatifu yosefu rejea kwenye harusi ya kana tunaambiwa kwamba siku ile Yesu alikuwepo pale harusini, na mama yake alikuwepo pamoja na ndugu zake wote na wote walitajwa majina lakini Yosefu hakutajwa .hii inadhihirisha kwamba mtakatifu Yosefu hakuwepo hata wakati huo ,na ilikuwa ni vigumu kwa yeye kutokuwepo kama mama yake Yesu mwenyewe amehudhuria
Pia harusi ya kana ni moja kati ya matukio yaliyo tokea mwanzoni kabisa mwa utume wa yesu .ndiyo maaana tunathibitisha kwamba Yosefu alikufa mapema hata kabla ya Yesu kuanza kazi ya utume
# je sisi wakatoliki tunamwabudu Bikira Maria?
Jibu la swali hili ni hapana kwani yeye ni mwombezi wetu huko mbinguni na anatupatanisha sisi na mwanaye Yesu kristu kwa kuwa sisi tulimkosea yeye kwa dhambi zetu na kwa kumuua yeye
Pia mtu anayesema kuwa sisi wakatoliki tunamwabudu Bikira Maria si ajabu akawa hajafahamu maana halisi a sala
Sala ni mazungumzo kati ya mwanadamu na mungu kwa njia mbalimbali. Tunaweza kusema sala zimegawanyika katika makundi matatu
i. Sala za maombi
ii. Sala za kuabudu.
iv. Sala za sifa
hata nyimbo tunazomwimbia mungu ni za aina tatu tu za kusifu za kumwabudu ama kumshukuru kwa mengi anayotujalia
lakini ni sala mbili tu tunazozipitisha kwa mama maria sala za maombi na sala za sifa , sala za kuabudu huwa tunazisali kwa Mungu tu ,hakuna sala ya kuabudu tunayompa bikira maria kwani ni mungu pekee anayepaswa kuabudiwa kwa kuwa yeye ndiye pekee aliyetuumba ,
hivyo tunaweza kusema kwamba sisi wakatoliki hatumwabudu Bikira Maria bali tunamheshimu tu kama mwombezi wetu
ikumbukwe kwamba nia ya Mungu ya kumtuma mwanaye wa pekee Yesu kristu ilikuwa ni kwaajili ya kutupatanisha na yeye ili tuwe karibu naye baada ya kumkosea kwa kutenda dhambi. Lakini baadala ya sisi binadamu kuitumia nafasi hiyo vizuri tulijikuta tukimkosea hata huyo mpatanishi wetu yaani Yesu kwa kumuua kwa kumsulubisha msalabani
hivyo bado tunahitaji nguvu nyingine ya maombi itakayotuweka karibu tena na huyo Yesu itakayokuwa ikituombea daima kwa mungu wakati sisi tusipoweza kujiombea ,ndiyo maaana sisi tunakimbilia kwa mama yake Yesu ili atuweke jirani tena na mwanaye kwa sala na maombi yake
kujua umuhimu wa maombi yake kwa Mungu chukulia mfano wa maisha yetu ya kila siku binadamu ,kila mara tunapokoseana na mtu Fulani huwa tunafanya juhhudi zote kupatana tena na mtu tuliyemkosea …fikiria kwamba umetenda kosa kwa mtu Fulani na urafiki wenu umedhoofika kiasi cha kukusa maelewano kati yenu .hivyo kupelekea wewe kushindwa kusaidiwa ama kupata msaada kutoka kwa mtu uliyemkosea. Unajaribu kuurudisha urafiki lakini inakuwia vigumu kwa kuwa ni wewe ndiwe uliyemkosea. Nadhani njia inayotumika na binadamu wengi ni kumtafuta mtu wa karibu wa uliyemkosea ama rafiki na kumuomba akupatanishe na uliyemkosea ama akusaidie shida Fulani unayohitaji kutoka kwake ili uweze kupatana naye haraka
hivyo ndivyo sisi tunayempenda Bikira Maria tunavyofanya kwa mungu , yaaani kwa kutambua makosa na dhambi tulizomfanyia mungu na kwamba tumemkasirisha yeye ,hivyo kufanya wakati mwingine juhudi za maombi yetu wenyewe kuchelewa ama kushindwa kupata msaada kutokana na makosa tuliyomtendea mungu na kama haitoshi bado tukamkosea na mpatanishi wetu yesu kristu
ndiyo maaana tunakimbilia msaada wa maombi ya Bikira Maria na watakatifu wengine wote ili yeye atuombee na kutupatanisha kwa mungu na mwanaye yesu kristu kwa kuwa yeye ni mtakatifu ,mbarikiwa na amejaliwa neema na Baraka nyingi .pia tunamkimbilia yeye kwa kuwa ndiye aliyetuletea mkombozi wetu yesu kristu na mwanae hawezi kumkatalia jambo lolote
Usiogope kumpenda sana Mama Maria kwani hata ukimpenda huwezi kumpenda Zaidi kama Yesu mwenyewe alivyompenda .Wala Yesu hatakuhukumu kwa kosa la kumpenda mama Yake kwani ni yeye mwenyewe aliyempenda kwanza kwa kumchagua yeye awe mama yake wakati alipokuwa anapanga kuja duniani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni